Habari Za Un

Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe

Informações:

Sinopsis

Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni Zahra Salehe, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania.