Habari Za Un

09 MEI 2024

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika kazi za Zahra Salehe na timu yake ya ICCAO nchini Tanzania katika kusongesha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza na asasi za kiraia Nairobi Kenya, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki. Leo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia umeng’oa nanga mjini Nairobi Kenya ukiwaleta pamoja washiriki takriban 1500 kutoka kila kona ya dunia wakifanya majadiliano ya awali na kutoa takwimu kuelekea mkutano wa wakati ujao utakaofanyika New York Marekani mwezi Sepemba mwaka huu. Umoja wa Mataifa Kenya ndio mwenyeji wa mkutano huo ambapo Mratibu Mkazi wa Umoja huo nchini humo Dkt. Stephen Jackson amesema taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa mstari wa mbele kwenye kusongesha ushirikiano wa kimataifa tangu uhuru wake.Huko Gaza takriban watu 80,000 wamekimbia Rafah tangu Jumatatu wiki hii wakati mashambulizi ya Israel yakishika kasi usiku kucha kuamkia leo ndani na katika viunga vya