Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Kabila aondolewa kinga ya kushtakiwa na Seneti ya DRC, Lissu arejeshwa mahakamani Tanzania
29/05/2025 Duración: 20minMiongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; Bunge la seneti nchini DRC lapiga kura ya kumuondolea kinga rais mtaafu Joseph kabila, Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, wafukuzwa nchini Tanzania. Kwingineko, Mamlaka nchini Libya zagundua miili 58 iliohifadhiwa kwa muda katika chumba cha kuhifadhi maiti na Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu awatuhumu viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Canada kwa kuwapa nguvu kundi la Hamas.
-
DRC: Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini
22/05/2025 Duración: 20minMakala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini kusaidia kuleta amani na utulivu Mashariki mwa nchi hiyo na pia serikali ya Uganda yawasilisha mswada tata bungeni kuruhusu kesi za kiraia kupelekwa kwenye Mahakama ya kijeshi. Taarifa zingine ambazo utaziskia ni uongozi wa kijeshi nchini Mali wasitisha sheria kuhusu vyama vya siasa nchini humo na Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya wajumbe wa Ukraine na Urusi yamefanyika wiki hii nchini Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022.
-
Robert Francis Prevost achaguliwa kumrithi Papa Francis na kuchukua jina la Papa Leo XIV
22/05/2025 Duración: 20minMakala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Mmarekani Robert Francis Prevost, achaguliwa kuongoza kanisa katoliki duniani, akichukua jina la Papa Leo wa kumi na nne. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, chatumbukia katika sintofahamu zaidi kufuatia baadhi ya waliokuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama, kutangaza kujiondoa kwenye chama hicho. Tarifa zingine utakazoskia, silaha za China zilizoagizwa na taifa la Falme za Kiarabu zimepatikana zikitumika na wapiganaji wa RSF nchini Sudan, na nchi jirani za India na Pakistan zashambiliana kwa silaha nzito na kuzua wasiwasi mkubwa katika maeneo ya mipakani.
-
Kuuawa kwa mbunge jijini Nairobi Kenya, Marekani kuzipatanisha Rwanda na DRC
03/05/2025 Duración: 20minMakala hii imeamgazia kuuawa kwa mbunge wa Kasipul Charles Ong'ondo Were, kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa kwa pikipiki katika barabara ya Ngong Jijini Nairobi, jumatano, kukamatwa kwa mlinzi wake kiongozi wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda, nao wawakilishi wa DRC na Rwanda wanaokutana Washington Marekani kusaini mkataba kuelekea makubaliano ya amani ya mashariki mwa DRC, siasa za Tanzania na kushambuliwa kwa kasisi wa kikatoliki na matukio kadhaa ya juma hili kutokea duniani