Gurudumu La Uchumi

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:59:41
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodios

  • Sehemu I: Madhara ya ushuru wa Trump kwa bara la Afrika na biashara ya dunia

    09/04/2025 Duración: 10min

    Kwa majuma kadhaa, mijadala mikali duniani kote kufuatia uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza ushuru zaidi wa bidhaa zinazoingia kwenye taifa hilo, mataifa ya Afrika yakiwa miongoni mwa waathirika, baadhi wakiwekewa ushuru wa hadi asilimia 50. Katika makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunadadavua na wataalamu athari za ushuru wa Trump kwa nchi za Afrika na biashara ya dunia kiujumla. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

  • Sehemu ya Pili: Uchakataji taka za plastiki kwa vijana

    02/04/2025 Duración: 10min

    Msikilizaji takwimu zinaonesha kuwa, ifikapo mwaka 2050, idadi ya watu barani Afrika itaongezeka kufikia bilioni 2.5, ambapo zaidi ya nusu ya watu hawa watakuwa ni vijana walio na umri wa chini ya 25. Hata hivyo Ujasiriamali wa vijana unaonekana kama suluhisho linalowezekana kwa changamoto hii. Msikilizaji juma hili nimebahatika kuwa na mgeni studioni nae si mwingine bali ni Kenneth Ochien’g, ambaye yeyé anajihusisha na uchakataji upya wa taka za plastiki kwa matumizi mengine.

  • Sehemu ya Kwanza: Uchakataji taka za plastiki kwa vijana

    26/03/2025 Duración: 10min

    Msikilizaji takwimu zinaonesha kuwa, ifikapo mwaka 2050, idadi ya watu barani Afrika itaongezeka kufikia bilioni 2.5, ambapo zaidi ya nusu ya watu hawa watakuwa ni vijana walio na umri wa chini ya 25. Hata hivyo Ujasiriamali wa vijana unaonekana kama suluhisho linalowezekana kwa changamoto hii. Msikilizaji juma hili nimebahatika kuwa na mgeni studioni nae si mwingine bali ni Kenneth Ochien’g, ambaye yeyé anajihusisha na uchakataji upya wa taka za plastiki kwa matumizi mengine.

  • Ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na Ufaransa

    19/03/2025 Duración: 10min

    Msikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.

página 2 de 2