Habari Za Un

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ yaamua juu ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu Gaza

    24/05/2024 Duración: 01min

    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo.Leo Kwa kura 13 dhidi ya 2 mahaka ya ICJ imeamua kwamba:1. Inathibitisha tena hatua za muda zilizoainishwa katika Maagizo yake ya tarehe 26 Januari 202 na 28 Machi 2024, ambayo yanapaswa kutekelezwa mara moja na kwa ufanisi2. Imeainisha hatua zifuatazo za muda kwamba : Taifa la Israeli, kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba juu ya Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, na kwa kuzingatia hali mbaya ya maisha inayowakabili raia katika Jimbo la RafahIsitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi, na hatua nyingine yoyote katika jimbo la Rafah ambayo yanaweza kusababishia kundi la Wapalestina Gaza hali hiyo ya maisha inayoweza kuleta uharibifu wa kimwili kwa ujumla au sehemu;Iendeleel kukiacha wazi kivuko cha Rafah  kwa utoaji usiozuiliwa kwa kiwango cha haraka cha hud

  • WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi

    24/05/2024 Duración: 02min

    Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na WHO ikijumuisha viashirikia vya afy na vinavyohusiana na imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2005.Ripoti yam waka huu kwa mujibu wa WHO imetathimini Zaidi ya viashiria 50 vinavyohusiana na afya kuanzia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mikakati kazi 13 ya WHO au GPW13.Ripoti inasema Janga la COVID-19 limefuta karibu muongo mmoja wa maendeleo katika kuboresha umri wa watu kuishi ndani ya miaka miwili tu. Kati ya 2019 na 2021, umri wa kuishi duniani ulipungua kwa mwaka 1.8 hadi miaka 71.4 ukirejea nyuma hadi kiwango cha mwaka 2012.”Pia ripoti imeongeza kuwa umri wa kuishi kwa afya duniani ulipungua kwa miaka 1.5 hadi miaka 61.9 mwaka 2021 ukiwa umerudi nyuma kwenye kiwan

  • Wanajeshi walinda amani wa UN wana majukumu mengine muhimu zaidi ya bunduki: TANBAT 7

    24/05/2024 Duración: 03min

    Zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika  Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA)

  • FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania

    24/05/2024 Duración: 03min

    Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu Mviwata FM ya Mkoani Morogoro amehudhuria Kikao hicho na kuandaa taaarifa hii. 

  • 24 MEI 2024

    24/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi ya ICJ ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, na  mifumo ya chakula nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo. Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021.Katika makaala zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na

  • Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”

    23/05/2024 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”

  • 23 MEI 2024

    23/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”  Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambalo ni tundu kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo, inayosababishwa mara nyingi na uchungu wa muda mrefu wakati wa kuelekea kujifungua, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na masuala ya kijinsia UNFPA Natalia Kanem amesema Fistula ya uzazi ni matokeo ya kusikitisha ya kushindwa kulinda haki za uzazi za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na ni lazima itokomezwe kwa watu wote. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Palestina Matthew Hollingworth ameandika katika ukurasa wake wa mtanda

  • Waathirika Garisa Kenya washukuru UNICEF kwa msaada wa fedha baada ya mafuriko

    22/05/2024 Duración: 03min

    Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa,maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la Norway kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo NORAD, Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti Ukame Kenya NDMA, na serikali ya Kaunti ya Garasa  kwani kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kujikimu kimaisha. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii

  • UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka

    22/05/2024 Duración: 01min

    Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana na kwamba makundi yenye silaha yamenyonga minyororo ya usambazaji, na kuweka mamilioni ya watoto katika hatari ya magonjwa na utapiamlo.Kila hospitali nchini Haiti imeripoti ugumu wa kupata na kutunza vifaa muhimu vya matibabu, kwani safari za ndege za kimataifa na za ndani za mizigo kutoka na kwenda katika viwanja vya ndege vya Port-Au-Prince zilirejea kufanya kazi hivi majuzi tu, zikiwa na uwezo mdogo na mrundikano mkubwa, kama ilivyokuwa kwa bandari kuu ambayo hapo awali ilikuwa mikononi mwa makundi yenye silaha."Mfumo wa afya wa Haiti uko karibu kuporomoka," Bruno Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti amesema akiongeza kwamba, "Mchanganyiko wa vurugu, ufurushaj

  • 22 MEI 2024

    22/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya kwa watoto nchini Haiti na simulizi afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kuhusu yanayoenndelea Gaza. Makala tnakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Makala inatupeleka Kaunti ya Garisa nchini Kenya ambako waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo ya hivi karibuni walio katika makambi za muda za wakimbizi wa ndani wanapokea msaada wa fecha na vocha kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake ikiwa

  • Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha - Nika Alexander

    22/05/2024 Duración: 02min

    Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Ni Nika Alexander kiongozi wa timu ya mawasiliano ya dharura kutoka WHO akieleza tofauti ya kwanza anayoona sasa akiwa amerejea kutoka Gaza ambapo wakati angali kule siku baada ya siku wakisikia mlio wa ndege basi bomu linaweza kuanguka dakika yoyote, wakati sasa ukiwa sehemu ambayo si ya vita akisikia mlio wa ndege pengine ni watu wanaendea likizo ni kama watu wa Gaza wanaishi kinyume na ulimwengu. Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kurejea Gaza Bi.Nika anasimulia hali ya kule. “Nilichoondoka nacho ni mawazo ya jinsi hali ilivyo mbaya kwa watu wa Gaza, jinsi hali ilivyo ngumu kwa watu wanaojaribu kuwasaidia watu wa Gaza na jinsi kulivyo hatari.” Amesema hospitali zinazofanya kazi ni chache na hazifanyi kazi kamili.“Kim

  • 21 MEI 2024

    21/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa mradi wa Cookfund, Elisabeth Ngoye amezungumza na Laurien Kiiza wa UNIC Dar es Salaam. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za afya, Gaza na Ukraine. Mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inaashiria ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa duniani, huku kukiwa bado na changamoto za Virusi Vya Ukimwi na homa ya ini. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X ameeleza wasiwasi mkubwa walio nao juu ya usalama wa wagonjwa na wafanyakazi waliokwama katika hospitali ya Al-Awda kaskazini mwa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Ukraine, limeeleza kuhusu wasiwasi mkubwa kutokana na hali inayozidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kwa Waukraine na kulazimishwa kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi mapya ya ardhin

  • Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer

    20/05/2024 Duración: 03min

    Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto katika kikosi na jamii ya wenyeji. Msimulizi ni Anold Kayanda

  • Baadhi ya wapalestina warejea kwenye nyumba zao zilizoathiriwa na mabomu baada ya kulazimishwa kuondoka Rafah

    20/05/2024 Duración: 02min

    Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.Baada ya kufika nyumbani kwake, Ibrahim Kamal Ibrahim Amtair anamuonesha mtoto wake mdogo wa kike box lililojaa bidhaa mbalimbali za msaada aliopokea kutoka WFP. Ibrahim ni mmoja wa watu waliokimbia makazi yao Khan Younis na kukimbilia Rafah baada ya amri ya Jeshi la Israel lakini baada ya Israel wiki iliyopita kutoa tena amri ya kuwataka kuondoka Rafah ameona hana tena pa kukimbilia na kuamua kurejea katika nyumba yake. Amekuta nyumba yake imeathirika vibaya na mabomu pamoja na risasi, baadhi ya maeneo hakuna madirisha wala milango huku kukiwa na

  • 20 MEI 2024

    20/05/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya sheria na uhalifu na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini CAR kufatilia kazi za walinda amani na mashinani tunakuletea ukumbe kuhusu ufugaji nyuki na thamana yao. Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.Makala inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa

  • ICC yawasilisha ombi kwa Baraza la Usalama la hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Netanyahu wa Israel

    20/05/2024 Duración: 02min

    Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Ni Karim Khan, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mapema leo alipotangaza kwamba anawasilisha maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na wa Israel kwa majaji wa mahakama hiyo ambao ndio watakaotoa uamuzi wa kutolewa kibali cha kukamatwa.Bwana Khan amesema kuna sababu za msingi za kuamini kwamba Yahya Sinwar wa Hamas, Mohammed Diab Ibrahim Al-Masri (Deif) na Ismail Haniyeh "wanawajibikia kijinai" kwa mauaji, kuangamiza na kuchukua watu mateka miongoni mwa uhalifu mwingine mwingi tangu mzozo wa Gaza ulipozuka kufuatia mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana 2023.“Pia kuna misingi ya kuridhisha ya kuamini kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa I

  • Orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa yatolewa na WHO

    17/05/2024 Duración: 01min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Katika taarifa iliyotolewa leo, WHO inafafanua kuwa usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawa hutokea pale ambapo bakteria, virusi, fangasi, na vimelea vingine vya magonjwa haviitikii tena dawa, hivyo kuongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa, watu kuugua na hata vifo.WHO inaeleza kwamba kwa sehemu kubwa hali hii ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa inasababishwa na matumizi mabaya ya dawa za viuavijumbe maradhi.Utafiti huu mpya uliotolewa leo unajumuisha uthibitisho mpya na maarifa ya kitaalamu ili kuongoza utafiti na maendeleo kwa ajili ya viuavijiumbemardahi yaani Antibiotics mpya na kuhamasisha uratibu wa kimataifa ili kukuza uvumbuzi.Baadhi ya bakteria sugu zilizotajwa ni Neisseria gonorrhoeae i

  • Uchumi wa dunia umeboreka kidogo ingawa Afrika bado kuna changamoto - Nelly Muriuki

    17/05/2024 Duración: 06min

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya katikati ya mwaka ya hali na mtazamo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo inaonyesha matarajio ya kiuchumi duniani yameboreka tangu utabiri uliotolewa Januari 2024, lakini mtazamo ni wa matumaini yanayohitaji tahadhari. Je, Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA ambao ndio wamezindua ripoti hiyo. 

  • 17 MEI 2024

    17/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics, na hali ya kibinadamu nchini Ukraine. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunaelekea nchini Afghanistan, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto.Makala inaturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulikozinduliwa ripoti ya nusu mwaka ya mtazamo wa ukuaji na matarajio ya uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024. Je Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezun

  • Mashirika ya kibinadamu yanahaha kuondoa watu huko Kharkiv Ukraine

    17/05/2024 Duración: 02min

    Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto. Video ya ofisi kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa, OCHAinaanza kwa kuonesha watu wakishuka katika bus, hawa ni raia walioondolewa huko Kharkiv ambako mapigano kati ya Ukraine na Urusi yanaendelea. Uokoaji unaendelea kupitia mabasi yanayoratibiwa na mashirika ya misaada ya kibinadamu, watu binafsi wanaojitolea na serikali za mitaa. Kwa mujibu wa OCHA kati ya tarehe 10 na 15 Mei, karibu watu 2,400 wamefanikiwa kuhamishwa na kuletwa kwenye kituo cha muda ambapo wanapokea usaidizi. Mmoja wa watu hao ni Bibi huyu aitwaye Valentyna anayetujuza hali ilivyokuwa huko alipotoka "Sisi kwetu ni Okhrimivka. Tunaishi pamoja na binti yangu ambaye ni mlemavu.  Kijiji chetu kilipigwa na

página 1 de 5