Sinopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodios
-
Fahamu kuhusu ugonjwa wa Endometriosis na changamoto za afya zinazofungamana nao
16/07/2024 Duración: 10minEndometriosis hutokea wakati tishu kwenye ukuta wa tumbo la uzazi zinapopatikana katika maeneo mengine ya mwili ikiwemo mapafu ,utumbo na hata ubongo Endemotriosis huwa na dalili zinazofanana magonjwa mengine ya uzazi na unaweza kubainika kupitia kipimo cha Laparoscopy ambapo tishu hizo zinachunguzwa moja kwa moja
-
Maandishi yenye tahadhari yatasaidia mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa
10/07/2024 Duración: 10minBidhaa za vyakula au vinywaji zikiwa na machapisho ya kuonesha kuwa vina sukari nyingi ,chumvi nyingi au mafuta mengi mnunuzi anakuwa na fursa ya kuchagua vema Watalaam wamesema lishe ni kiungo muhimu katika kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanazidi kuongezeka na kuwa mzigo kubwa kwa jamii na mifumo ya afya
-
Mashujaa wa kupambana na Vitiligo wana matumaini makubwa ya jamii kuwaelewa
10/07/2024 Duración: 09minJamii nyingi bado hazielewi kuwa ugonjwa wa Vitiligo hauwezi kuambukizwa kwa kutangamana ,kugusana au hata kushiriki mlo
-
Dunia yaadhimisha siku ya ugonjwa wa ngozi - Vitiligo
29/06/2024 Duración: 10minVitiligo ni hali ya ngozi ambapo madoa meupe au mabaka yanaonekana. Inaweza kuathiri mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na watoto na vijana. Sio hatari, si kama saratani ya ngozi au maambukizi unayoweeza kupata na kwa hiyo huwezi kuipata kutoka kwa mtu mwingine. Watu wengi wenye vitiligo wana afya nzuri. Baada ya muda, mabaka zaidi yanaweza kuonekana kwenye sehemu tofauti za mwili, hata kwenye nywele au ndani ya kinywa na pua. Mara nyingi huanza katika maeneo yaliyopigwa na jua. Takriban 1% ya dunia ina vitiligo