Siha Njema

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 4:01:18
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Episodios

  • Kupanga uzazi kwa kutumia njia za homoni na ile ya Kitanzi -Matatizo ya Afya kwa Wanawake

    24/12/2024 Duración: 10min

    Kwenye awamu yetu ya Kwanza tuliangazia njia za asilia walizokuwa wanatumia nyanya zetu kabla ya sayansi kuingia.Tukataja njia ya Kalenda,mipira ya kondomu na kumwaga mbegu za kiume nje ya njia ya uzazi almaarufu Withdrawal.Hivyo basi kwenye sehemu hii ya pili tutaangazia njia za homoni na zisizo za homoni na  ambazo asilimia kubwa ya wanawake wanatumia.Kama vile vidonge, vipandikizi ,sindano, na IUD.

  • Uzazi wa mpango kwa njia asilia

    17/12/2024 Duración: 09min

    Makala  haya yanaangazia upangaji kupanga uzazi, na jinsi linavyohusiana na afya ya mwanamke. Kupanga uzazi ni sehemu muhimu ya afya, kwani husaidia wanawake kudhibiti idadi ya watoto wanapokuwa nayo, na pia ina athari kubwa katika afya yao ya kimwili na kihisia.

  • Juhudi za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya eneo la Pwani ya Kenya

    13/12/2024 Duración: 10min

    Idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya katika umri mdogo imeongezeka

  • Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani

    09/12/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya, tutazungumza na watu muhimu kama vile mgonjwa wa UKIMWI, daktari, na mkunga anayeelimisha kuhusu jinsi ya kuzuia watoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wanapozaliwa. Pamoja, tutafahamu changamoto, mafanikio na hatua zinazochukuliwa katika vita hivi.

  • Dunia: Wahudumu wa afya waendelea kuuawa katika maeneo ya mizozo

    07/12/2024 Duración: 10min

    Umoja wa mataifa umeorodhesha mwaka 2024 kama mwaka hatari zaidi kwa wafanyikazi wa mashirika ya kimsaada Katika takwimu za UN ,wafanyakazi zaidi ya 200 wamewauwa katika mzoz wa Gaza na wengine zaidi ya 20 katika mzozo wa Sudan

  • Afya ya kujifungua na uzazi: Changamoto zinazotokea wakati wa kujifungua mtoto

    12/11/2024 Duración: 10min

    Idadi kubwa ya kina dada wameamua kuchagua  upasuaji kama njia rahisi ya kujifungua kwa sababu tofauti tofauti.Sehemu ya pili ya makala haya inaangazia ni kwa nini idadi hio inaongezeka kisha hali inakuaje pale kwenye chumba cha kujifungulia.Dakatari Lilian Nkirote kutokea hospitali ya Jacaranda jiji Nairobi anaelezea kwa kina.

  • Afya ya uzazi na kujifungua

    08/11/2024 Duración: 10min

    Makala ya siha njema wiki hii tunaangazia Afya ya uzazi na kujifungua na sio safari  nyepesi.Ni safari yenye  changamoto haba na furaha kwa wanawake na familia zao. Ni muhimu kwa kila mama mjamzito kufahamu hatua muhimu za kuhakikisha ustawi wa afya yake na ya mtoto anayemtarajia. Kupitia huduma bora za kiafya na ushauri wa wataalamu, wanawake wanaweza kufurahia safari ya uzazi kwa usalama na utulivu.

  • Juhudi za kikanda kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka

    29/10/2024 Duración: 08min

    Kumekuwa na mikakati maksudi katika nchi za Afrika kuwekeza katika utafiti kuhusu nyoka  na matibabu ya simu yake  Baadhi ya mikakati hiyo ni utafiti wa kuwa na aina moja ya dawa ambayo inaweza kutumika katika nchi za Afrika Mashariki vile vile kuelimisha jamii kuhusu huduma za kwanza sahihi kuwasaidia wagonjwa na namna ya kuzuia madhara zaidi kutokana na sumu ya nyoka.

  • Kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka katika ukanda wa Afrika

    22/10/2024 Duración: 10min

    Kungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu  hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa  kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSFMSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.

  • ICRC yapambana kutoa huduma za afya za dharura ndani ya saa 96

    08/10/2024 Duración: 10min

    Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC mara nyingi hubidi kuhudumu katika maeneo yenye mizozo kutoa huduma za dharura ,msaada wa kibinadaam ikiwemo afya Ili kukabiliana na changamoto za kuafikia malengo yake ya kutoa huduma za afya za dharura katika uwanja wa vita ,maeneo yenye majanga ,imebidi kufumbua mbinu ya kuwa na hospitali za muda ambazo zinajengwa kutumia hema na zinaweza kufanya kazi ndani ya saa 96ICRC inaendelea na mafunzo ya kuwaandaa wahudumu wa afya wanaohudumu katika mazingira hatarishi ,ili wapate kuhudumu ipasavyoMafunzo hayo yanatolewa kwenye hospitali halisi ambazo hutumika katika maeneo ya mizozo ,ambapo wahudumu hao hutakiwa kushughulikia mazingira tofauti ya dharuraMafunzo hayo yamefanyika nchini Kenya mara mbili ambapo wahudumu hao kutoka maeneo tofauti wanawekwa kwenye makundi na kutakiwa kutangamana na kushughulikia dharura tofauti kabla kuanza kutumwa kwenye maeneo ya mizozo

  • Ugonjwa wa Selimundu maarufu Sickle Cell unavyowaathiri wengi

    07/10/2024 Duración: 09min
  • Ubunifu kutatua changamoto za miundombinu kwenye usafi na maji taka

    24/09/2024 Duración: 10min

    Mashirika ya nchini Kenya  kwa ushirikiano na serikali za kaunti ,yamezindua  mfumo mpya na wa kisasa wa vyoo bunifu visivyotumia maji wala kuunganishwa na mabomba ya maji taka Hatua Ambayo imeonekana kupunguza msambao wa magonjwa kama vile kipindupindu.

  • Ukosefu wa Ufahamu wa haki za afya ya uzazi ni kikwazo kikubwa ukanda wa Afrika

    17/09/2024 Duración: 10min

    Raia wengi bado hawawezi kufurahia haki zao za afya ya uzazi kutokana na ukosefu wa ufahamu Haki hizo ni pamoja na haki ya kuwa mzazi au la,kupata habari kuhusu afya ya uzazi ,kupata huduma bora za uzazi ,kushiriki mapenzi kwa njia stahiki na kuhudumiwa katika vituo vya afya kwa heshima

  • Matatizo ya kupata uja uzito miongoni mwa wanafamilia yanazidi kuongezeka

    03/09/2024 Duración: 10min

    Ripoti nyingi  zinaonesha wanawake pamoja na wanaume wanakabiliwa na changamoto za uzazi Wanandoa nyingi wanalazimika kukaa miaka mingi kabla kupata watoto ,kitu ambacho bado kinazingatiwa na jamii za Afrika kuwa ukamilifu katika kila ndoa au familia.Daktari bingwa wa uzazi dkt Dennis Miskella anaeleza  juhudi za kutafuta mtoto zinastahili kuwa ushirikiano kati ya mke na mumeweBaadhi ya sababu zinazohusishwa na hali hii ni kushiriki tendo la ndoa visivyo ,athari za baadhi ya mbinu za kupanga uzazi ,uvutaji sigara na pia unene wa kupitiliza

  • Wanawake wawafuga samaki kukwepa msambao hatari wa Ukimwi ziwa Victoria

    28/08/2024 Duración: 09min

    Mashirika ya kiraia yanayofanya kazi maeneo ya Kisumu nchini Kenya wanawasaidia wanawake kuachana na mpango wa kuuza miili yao ili kupata samaki Tabia hiyo inayofahamika kama ngono samaki kwa wakazi imekuwa ikichangia msambao wa virusi vya HIV

  • WHO imetoa mwongozo wa kupambana na MPOX katika mataifa ya Afrika

    20/08/2024 Duración: 10min

    Mikakati ambayo WHO inahimiza nchi za Afrika kukumbatia ni ubadilishanaji wa taarifa kuhusu ugonjwa wa Mpox ,ubainishaji sahihi na kampeni za chanjo Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,kuna hofu ya msambao hatari wa MPox  unaohuishwa na vitendo vya ngonoWatalaam wa afya nchini DRC pia wanahimiza uhamasisho zaidi kuhusu ugonjwa huo ambao umesababisha vifo zaidi ya 500

  • MPOX yatangazwa janga la dharura la kiafya baada ya kasi ya maambukizi kuzidi

    20/08/2024 Duración: 09min

    Shirika la afya duniani ,WHO na taasisi ya kudhibiti magonjwa ya umoja wa Afrika ,CDC zililazimika kuchukua uamuzi mzito wa kutangangaza MPOX dharura ya kiafya Mataifa 16 ya Afrika kati ya 55 yameripoti visa vya MPOX mwaka huu ,CDC ikisema maambukizo yamepanda hadi asilimia 160 mwaka huu ukilinganishwa na mwaka 2023Virusi vya MPOX vimeripotiwa kujibadilisha  na kwa sasa msambao hatari wa virusi sugu zaidi unahusishwa na ngono

  • Bidhaa mpya za tumbaku zinauzwa kwa mwoneko bora, ladha ya kuvutia kuficha madhara yake

    06/08/2024 Duración: 09min

     Kuuza bidhaa za tumbaku za kisasa ,kama bidhaa zisizo na madhara ,kutumia ladhaa tamu na kutumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa hizi ni mbinu ambao kampuni za kutengeneza tumbaku zinatumia kuwavutia vijana na kuwa wateja wao wa kudumu. Kampuni hizi zinafadhili pia utafiti ambao unakinzani na utafiti wa taasisi za afya kuhusu madhara ya Tumbaku.Isitoshe kampuni hizi zinazalisha bidhaa ambazo mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya moja .

  • Mbinu fiche zinazotumia sekta ya kuzalisha tumbaku kuendelea kudumu soko

    01/08/2024 Duración: 10min

    Kumeshuhudia juhudi makhsusi kutoka sekta ya Tumbaku zinazopinga sheria zinazodhibiti Tumbuka kama vile kupitia ushuri au sheria zenye adhabu kali Sekta hii pia imeonekana kurubuni serikali tofauti kwa kutoa msaada bila wao kufahamu lengo la sekta hiyo. Aidha kuna tafiti za kisayansi zinazofadhiliwa na sekta hii kukabili sayansi zinazorodhesha tumbaku na bidhaa za sigara kuwa zenye madhara makubwa ya kiafya

  • Simulizi kuhusu ugonjwa wa Endometriosis unaowasababishia wanawake maumivu

    24/07/2024 Duración: 10min

    Ugonjwa wa Endometriosis hudhihirika msichana anapovunja ungo na huja na maumivu makali kabla ,wakati na hata baada ya hedhi Lilian Leley ameishi na maumivu hayo kwa zaidi ya miaka thelathini.Amefanya upasuaji mara mbili na anatazamiwa kwenda kwenye operesheni nyingine hivi karibuni katika kujaribu kutafuta tiba ya ugonjwa wa EndometriosisAnasimulia masaibu yake ,ambapo anasema ndani ya mwezi huenda ni mzimu tu kwa siku 10

página 1 de 2