Jukwaa La Michezo

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • Uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Tennis barani Afrika

    28/10/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika kupata viongozi wapya wa Shirikisho la mchezo wa Tenisi, uchambuzi wa fainali ya kombe la dunia la raga, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury na Francis Ngannou, mechi za kufuzu olimpiki ya mwaka kesho kwa kina dada, Ligi Kuu ya soka Afrika, debi la Manchester na El Clasico na mchezaji wa Newcastle Sandro Tonali kupigwa marufuku ya miezi kumi kwa kujihusisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu.

  • Raga: Afrika Kusini na New Zealand kuchuana fainali ya kombe la dunia

    22/10/2023 Duración: 23min

    Tumekuandalia uchambuzi kuhusu fainali inayotarajiwa kati ya Afrika Kusini na New Zealand, kuwania taji la kombe la dunia katika mchezo wa raga lakini pia kuendelea kwa michuano mipya ya soka ya ligi ya Afrika.

  • CAF yatangaza droo ya hatua ya makundi, michuano ya klabu bingwa na Shirikisho

    07/10/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika, Gor Mahia yaibuka na ushindi kwenye debi la mashemeji, uchambuzi wa matokeo ya mechi za klabu bingwa ulaya, Kombe la Dunia la mwaka 2030 kuandaliwa kati ya mataifa sita na Pogba kupatikana ametumia dawa za kusisimua misuli katika kipimo cha pili.

  • Afrika Mashariki kuwa wenyeji wa AFCON 2024

    30/09/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika Mashariki kuteuliwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027, hatua ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya wanawake mwaka 2024, raundi ya mwisho kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Kombe la dunia la raga, linaloendelea nchini Ufaransa.

página 2 de 2