Jukwaa La Michezo

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • Mashindano ya barani Afrika mwaka 2023 yakamilika nchini Ghana

    23/03/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na Kenya kuongoza chati ya medali Afrika Mashariki katika mashindano ya Afrika, Shirikisho la soka Cameroon yaondoa kashfa ya udanganyifu wa miaka dhidi ya Nathan Doualla, mkurugenzi mwandalizi wa WRC Safari Rally Jim Kahumbura ajiuzulu, droo ya soka mashindano ya Olimpiki na Nottingham Forest kupokonywa alama nne kutofuata sheria wa fedha Uingereza.

  • CAF CL: Tp Mazembe, Yanga na Simba wafahamu wapinzani wao wa robo fainali

    16/03/2024 Duración: 23min

    Karibu katika makala ya jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi tukianzia na droo ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika, mashindano ya bara afrika pamoja na droo ya robo fainali katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.

  • Ndondi : Anthony Joshua amshinda Francis Ngannou katika raundi ya pili

    09/03/2024 Duración: 24min

    Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kushindwa kwa mwana masumbwi Francis Ngannou na Anthony Joshua,kuanza kwa mashindano ya 13 ya bara Afrika nchini Ghana pamoja na Paris Saint Germain kufuzu katika robo fainali michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

  • Kenya kujenga uwanja mpya kwa ajili ya michuano ya Afcon mwaka 2027

    02/03/2024 Duración: 23min

    Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kujengwa kwa uwanja mpya wa michezo nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika pamoja na taifa la ufaransa kukamilisha ujenzi wa kijiji kitakachotumiwa na wanariadha katika michezo ya olimpiki.

  • Mashindano ya Tour du Rwanda mwaka 2024 yamekamilika hii leo jijini Kigali

    25/02/2024 Duración: 22min

    Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tunaangazia kukamilika kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mashindano ya mchezo ya gofu Magical kenya open pamoja na klabu ya Yanga na Tp Mazembe kufuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika.

  • Mashindano ya Tour du Rwanda kuanza hapo kesho katika mji wa Kigali

    17/02/2024 Duración: 24min

    Karibu katika makala ya Jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi ikiwemo kuanza kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mazungumzo ya kipekee na waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro pamoja na  kupigwa marufuku mechi nne kwa mchezaji wa timu ya taifa ya senegal Kreppin Diatta.

  • AFCON 2024 : DRC kucheza dhidi ya Afrika Kusini katika nafasi ya tatu

    10/02/2024 Duración: 25min

    Miongoni mwa taarifa kuu tutakazozianhazia ni pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya bara afrika AFCON kuchezwa hapo kesho mwenyeji Ivory coast wakipambana na Nigeria. Mchezaji wa tenisi nambari moja barani afrika Ons Jabeur kushindwa katika mashindano ya Abu dhabi na fainali ya kombe la mataifa ya bara Asia kuchezwa leo.

  • AFCON 2024: DRC na Nigeria zatinga hatua ya nusu fainali

    03/02/2024 Duración: 23min

    Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na taifa la DR Congo pamoja na Nigeria kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michuano ya  kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Dereva wa magari ya langalanga Lewis Hamilton kuhamia katika timu ya Ferrari kutoka Mercedes mwaka 2025.

  • AFCON 2024: Michuano ya hatua ya 16 bora kuanza

    27/01/2024 Duración: 23min

    Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya hatua ya 16 kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Mashindano ya mchezo wa mikono bara Afrika yanayoendelea kule Misri na Aryna Sabalenka  kushinda mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanawake.

  • Mataifa ya Afrika yaendelea kupambana kutafuta taji la AFCON

    20/01/2024 Duración: 23min

    Tunaendelea kukuletea uchambuzi wa michuano ya soka kuwania ubingwa kwa mataifa ya Afrika, inayoendelea nchini Cote Dvoire. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, pia zinapambana kuwania taji hilo. Ungana na wachambuzi wetu Jason Sagini, George Ajowi na Jason Sagini akiwa mjini San Pedro.

  • Michuano ya AFCON yaanza nchini Cote Dvoire, nani ataibuka mshindi ?

    13/01/2024 Duración: 23min

    Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. Wachambuzi wetu Paul Nzioki, George Ajowi na Jason Sagini, akiwa  Abidjan, wnachambua.

  • CAF yaongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa AFCON 2024

    06/01/2024 Duración: 23min

    Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa  Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa michuano ya AFCON, itakayoanza Januari 13 nchini Cote Dvoire,  Bondia wa DRC Martin Bakole aomba mchango wa fedha kushiriki mechi za mkanda wa WBA, matokeo ya Mapinduzi Cup na kombe la Amani visiwani Zanzibar na Brazil yamfuta kazi kocha Fernando Diniz.

  • Timu za Afrika zaanza kutangaza vikosi kuelekea AFCON 2024

    30/12/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa vikosi vya mwisho vilivyotangazwa na mataifa kadhaa kuelekea AFCON ya mwaka 2023 itakayoanza Januari 13, 2024, raia wa Rwanda Clare Akamanzi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NBA Africa, Guy Bukasa atangazwa kocha mpya wa AS Kigali, rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach atangaza mikakati ya kujumuisha michezo ya kielektroniki e-sports kwenye Olimpiki na kocha Carlo Ancelotti atia saini mkataba mpya klabuni Real Madrid.

  • Kenya yaibuka bingwa wa mashindano ya Tong Il Moo Do

    23/12/2023 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kuhifadhi taji lake la Tong Il Moo Do kwa mara ya 11, mkenya Angella Okutoyi ashinda dhahabu mbili kwenye tenisi ya kimataifa ya W25, uchambuzi wa matokeo ya mechi za Klabu bingwa Afrika wiki hii, Man City kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu bingwa Duniani kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Ulaya kupinga uamuzi wa FIFA na UEFA kuzuia kuanzishwa kwa Ligi mpya ya Ulaya kuwa kinyume na sheria. 

  • Mashindano ya Kimataifa ya Tong-Il-Moo-Do yafanyika nchini Kenya

    16/12/2023 Duración: 21min

    Kenya yaandaa makala ya 11 ya michuano ya kimataifa ya mchezo wa Tong-Il-Moo-Do jijini Mombasa. Uganda ndio washindi wa CECAFA katika mechi za kufuzu kwa michuano ya CAF ya Shule za Afrika. Al Ahly waishinda Al-Ittihad kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Kisha Paris Saint - Germain yatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.

  • Messi ashinda tuzo ya Ballon d'Or tena

    04/11/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa yale tunayojadili ni pamoja na tuzo za wachezaji bora barani Afrika mwaka huu katika mchezo wa soka, timu ya taifa ya Uganda Cranes kupata kocha mpya, mechi za soka kufuzu michezo ya Olimpiki Paris 2024 miongoni mwa wanawake, Lionel Messi kushinda tuzo ya nane la Ballon d'Or, miongoni mwa mengine.

  • Uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Tennis barani Afrika

    28/10/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika kupata viongozi wapya wa Shirikisho la mchezo wa Tenisi, uchambuzi wa fainali ya kombe la dunia la raga, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury na Francis Ngannou, mechi za kufuzu olimpiki ya mwaka kesho kwa kina dada, Ligi Kuu ya soka Afrika, debi la Manchester na El Clasico na mchezaji wa Newcastle Sandro Tonali kupigwa marufuku ya miezi kumi kwa kujihusisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu.

  • Raga: Afrika Kusini na New Zealand kuchuana fainali ya kombe la dunia

    22/10/2023 Duración: 23min

    Tumekuandalia uchambuzi kuhusu fainali inayotarajiwa kati ya Afrika Kusini na New Zealand, kuwania taji la kombe la dunia katika mchezo wa raga lakini pia kuendelea kwa michuano mipya ya soka ya ligi ya Afrika.

  • CAF yatangaza droo ya hatua ya makundi, michuano ya klabu bingwa na Shirikisho

    07/10/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika, Gor Mahia yaibuka na ushindi kwenye debi la mashemeji, uchambuzi wa matokeo ya mechi za klabu bingwa ulaya, Kombe la Dunia la mwaka 2030 kuandaliwa kati ya mataifa sita na Pogba kupatikana ametumia dawa za kusisimua misuli katika kipimo cha pili.

  • Afrika Mashariki kuwa wenyeji wa AFCON 2024

    30/09/2023 Duración: 23min

    Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika Mashariki kuteuliwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027, hatua ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya wanawake mwaka 2024, raundi ya mwisho kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Kombe la dunia la raga, linaloendelea nchini Ufaransa.

página 1 de 2