Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Vitendo vya utekaji kuongezeka Nigeria na baadhi ya nchi za Afrika ya kati
24/11/2025 Duración: 10minMsikilizaji juma lililopita watu wenye silaha waliwateka wanafunzi zaidi ya 300 pamoja na waalimu katika shule moja kwenye jimbo la Niger nchini Nigeria, tukio linalojiri siku chache tangu kutekwa kwa wanafunzi wengine 25 katika shule ya wasichana kwenye jimbo la Kebbi pia huko Nigeria. Vitendo vya utekaji wa watoto vinazidi kuongezeka katika nchi za Afrika magharibi na kati. Nini kifanyike kukomesha vitendo hivyo Afrika?Je taifa lako linashuhudia utekaji wa watoto? Ungana na Ruben Lukumbuka
-
Maoni ya mskilizaji kuhusu matangazo yetu
23/11/2025 Duración: 10minKila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi ya kuchangi mada yoyote kuhusu taarifa na vipindi vyetu au kile kinafanyika hapo ulipo. Skiza maoni ya waskilizaji juma hili.
-
Tanzania : Rais Samia amuteua mwanawe kuwa naibu waziri
20/11/2025 Duración: 09minTunajadili hatua ya viongozi kadhaa wa Afrika akiwemo rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wamewateua watu wa familia zao katika nafasi za serikali, hali hii ikionekana kwenda kinyume na maadili ya kazi. Tunakuuliza Je, uteuzi wa ndugu serikalini ni sahihi au si sahihi? skiza Makala haya
-
Kenya : Vyama vya kisiasa vina umuhimu kujenga demokrasia
20/11/2025 Duración: 09minKatika makala haya tunaangazia nchi ya Kenya ambapo chama cha ODM kilichokuwa cha waziri mkuu wa zamani hayati Raila Odinga, kimeadhimisha miaka 20 tangu kuasisiwa kwake. Tunauliza je vya kisiasa vina mchango gani katika kuimarisha demokrasia hapa Afrika? Skiza makala haya.
-
Tanzania : Chakera kuwa mpatanishi
19/11/2025 Duración: 09minAliyekuwa rais wa Malawi , Lazarus Chakwera kuteuliwa na Jumuiya ya madola kuwa mpatanishi wa mzozo wa kisiasa nchini Tanzania, hasa baada machafuko ya kipindi cha uchaguzi. Tunakuuliza , unafikiri rais Chakwera atafanikiwa kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Tanzania.
-
Ajali za barabarani zazidi kuwaua raia Africa
17/11/2025 Duración: 09minUlimwengu umeadhimisha siku ya kumbukumbu kwa waathiriwa wa ajali za barabarani. Takwimu za umoja wa mataifa zinaonyesha kuwa, duniani kote, watu zaidi ya milioni moja hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, na millioni hamsini kujeruhiwa. Nini kifanyike kupunguza ajali za barabarani. Skiza makala kufahamau maoni ya mskilizaji zetu.
-
Trump atishia kutumia jeshi la Marekani kupambana na wanajihadi wanaowauwa Wakiristo nchini Nigeria
07/11/2025 Duración: 09minKatika makala ya Habari Rafiki hii leo tunazungumzia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kutumia jeshi la nchi yake kupambana na wanajihadi wanaowauwa Wakiristo nchini Nigeria. Kauli hii imewakasirisha viongozi wa Nigeria, ambao wanasema serikali nchini humo, haiungi mkono unyanyasaji wa kidini. Tumemuuliza msikilizaji anazungumzia vipi mpango wa huu wa Trump na ni nini kinaweza kufanyika kumaliza mauaji ya kidini nchini Nigeria.
-
Tanzania : Maoni ya waskilizaji kuhusu uchaguzi wa Tanzania
01/11/2025 Duración: 09minNini kilikukera kuhusu uchaguzi wa Tanzania ? Skiza maoni ya waskilizaji wetu.
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu matukio ya juma hili
31/10/2025 Duración: 10minKila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote kuhusu matukio ya dunia. Skiza maoni ya waskilizaji juma hili.
-
Kenya : Mitandao ya kijamii inasababisha matatizo
29/10/2025 Duración: 10minGazeti la The Star nchini Kenya limewahi chapisha ripoti inayoonesha namna mitandao ya kijamii inavyoathiri watu kwa kusababisha wasiwasi, matatizo ya afya ya akili na athari nyinginezo. Tunakuuliza Je, maisha ya mitandao yanatusaidia kama jamii au yanatuumiza? skiza maoni ya waskilizaji wetu.
-
Tanzania : Raia wajitokeza kumchagua rais na wabunge
29/10/2025 Duración: 10minShaba yetu katika makala haya inalenga nchi ya Tanzania ambapo raia wameshiriki uchaguzi kumchagua rais na wabunge. Je, unauzungumziaje uchaguzi wa Tanzania? Haya hapa maoni ya waskilizaji.
-
Djibouti : Laondoa ukomo wa kuwania urais
27/10/2025 Duración: 09minDjibouti limekuwa taifa la hivi punde kuondoa rasmi kikomo cha umri wa rais , hatua inayotoa fursa kwa rais Ismail Omar Guelleh kugombea muhula wa sita katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Aprili mwaka ujao. Awali Katiba ya nchi hiyo ilikuwa inamzuia rais kugombea tena baada ya kufikisha miaka 75. Hali hii pia imeonekana kwenye mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki kama vile Uganda. Skiza mahakala haya kuskia maoni ya waskilizaji.
-
KILA SIKU YA IJUMAA KWENYE KPINDI CHA HABARI RAFIKI NI MADA HURU
24/10/2025 Duración: 10minLeo ni siku ya mada huru. Tunakupa nafasi kuzungumzia suala lolote ambalo limetokea nchini mwako wiki hii Unaweza pia kujadili kile ambacho umekisikia katika matangazo yetu ya wiki hii kwenye redio.
-
WANASAYANSI VIONGOZI WAKUTANA AFRIKA KUSINI KUJADILI AFYA BILA UFADHILI WA NJE
23/10/2025 Duración: 10minViongozi wa dunia, wataalam wa Afya na wanasayansi wanakutana Afrika Kusini siku chache kabla kikao cha G20, ili kuanganzia kuhusu njia za kufadhili afya bila kutegemea ufadhili wa kigeni.Tumemuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu uwezo wa mataifa ya Afrika kufadhili miradi ya afya?
-
Mateka wa Israeli waliokuwa wanashikiliwa na Hamas waachiwa huru huko Gaza
13/10/2025 Duración: 10minHivi leo viongozi wa dunia akiwemo rais wa Marekani, Donald Trump, wanakutana Misri kujadili mustakabali wa eneo la Gaza, baada ya makubaliano ya kihistoria ya wiki iliyopita. Makubaliano haya yameshuhudia kuachiwa kwa mateka, wafungwa na kusitishwa kwa vita vya Gaza. Tunakuuliza, unaamini makubaliano kati ya Hamas na Israel safari hii yatadumu?Nini cha zaidi kifanyike?Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
-
Tuzo ya nobeli kutolewa ijumaa wiki hii
09/10/2025 Duración: 09minMsikilizaji kesho Ijumaa oktoba 10 kamati inayotoa tuzo za kimataifa za Nobel itamtangaza mshindi, wakati huu watu wengi wakiwa wamempendekeza rais wa Marekani Donald Trump kutokana na mchango wake wa kutafuta amani mashariki ya kati, hata hivyo wadadisi wanasema kiongozi huyo hawezi kupewa tuzo hiyo. Unafikiri ni Kiongozi gani anastahili kupewa tuzo hii mwaka huu na kwanini? Ungana nami Ruben Lukumbuka, mubashara kutoka studio namba mbili hapa karibu tuandamane hadi tamati.-
-
Vitendo vya utekaji nyara kuongezeka Afrika mashariki
09/10/2025 Duración: 10minHabari rafiki ya jumatano octoba 08 imeangazia vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki, hivi karibuni nchini Uganda wanaharakati wawili kutoka nchini Kenya walikamatwa baada ya kuhudhuria mkutano wa kisiasa wakati nchini Tanzania, aliyekuwa balozi wa nchi hiyo huko Cuba Humphrey Polepole alitekwa na watu wasiojulikana na mpaka sasa hajulikane alipo. Sikiliza makala hii kupata mengi zaidi
-
Waasi wa M23 huko DRC wajiimarisha katika kutengeneza serikali mbadala
07/10/2025 Duración: 10minWaasi huko mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameendelea kujiimarisha kiutawala, kisiasa na kimiundo mbinu katika kujenga barabara, kutangaza orodha ya mawakili, hatua inayodhihirisha kuwa waasi hao wanaendea kutengeneza serikali mbadala na ile ya Kinshasa. Makala ya habari rafiki inaangazia hatua hiyo
-
Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila ahukumiwa kifo, maoni ya wasikilizaji
01/10/2025 Duración: 10minMahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imemhukumu rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila Kabange adhabu ya kifo bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali. Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anaungana na wasikilizaji wa Idhaa kupata maoni yao kuhusu kesi hii, makinika kwa kusikiliza makala hii.-
-
Serikali ya DRC kusitisha leseni za makanisa na taasisi za kisheria
30/09/2025 Duración: 10minSerikali ya DRC kupitia wizara ya sheria imesitisha utoaji wa leseni za Makanisa, katika kupambana na Rushwa! kwa maoni yako unaamini kusitisha utoaji wa leseni kutasaidia kupambana na rushwa? Hali ya rushwa ikoje katika taasisi za umma nchini mwako? Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka pamoja na wasikilizaji wetu wanajaribu kupata jibu kwa maswali hayo